Thursday, October 3, 2019

ZIARA YA KASA ZOO


Ilikua siku ya tarehe 30/05/2019 siku ya Ijumaa, ambapo walimu, wanafunzi na wafanyakazi wote wa shule ya Mwanza Istiqaama Pre & Primary School walijumuika katika safari ya kimasomo kuelekea "KASA ZOO" jijini Mwanza. 

Ilikua safari nzuri na salama ambapo wanafunzi walifurahi pamoja na walimu wao na kujifunza vitu mbali mbali vinavyohusu wanyama pori na wanyama wanaofugwa nyumbani. Wanafunzi walipata kuona kwa mara yao ya kwanza wanyama wakubwa na wadogo wa porini na kustaajabu sana! Waliona farasi, ngamia, punda milia, kobe, sungura, nyoka wakubwa na wadogo, ndege aina nyingi na namna waoishi.

Pamoja na yote hayo, wanafunzi wetu walipata sehemu nadhifu na ya utulivu iliyo wawezesha kujumuika na walimu wao kula na kunywa na kupeana zawadi, pia wanafunzi walipa fursa ya kuuliza maswali mbali mbali yanayohusu wanyama, mfano mwanafunzi mmoja aliuliza 
"Yule mamba kafa? Kiongozi wa ziara alimjibu kua mamba akishiba hulala hadi masaa 48!"
Ilikua safari nzuri sana, hizi ni baadhi ya picha zetu.






2 comments: