Karibu Mwanza Istiqaama Pre and Primary Schools
Shule tulivu yenye Mandhari tulivu yenye mvuto wa kipekee
Wanafunzi wakiwa Darasani
Mazingira yanayo ruhusu kusoma kwa utulivu. Mlete Mwanao Aelimike
Walimu wenye sifa stahiki.
Jiunge leo ujionee tofauti. Gharama zetu ni Rafiki kwa kila mtu.
Usafiri makini kwa Wanafunzi wetu
Usafiri salama, Dereva weledi walio bobea katika fani ya udereva na kujali mwanafunzi wakati wote
Karibu Mwanza Istiqaama Pre and Primary School
Faith Knowledge Success.
Tuesday, December 3, 2019
Tuesday, October 22, 2019
SHULE YETU
Mwanza ni miongoni mwa mikoa mizuri sana unaopatikana kaskazini mwa Tanzania, jiji la Mwanza linajuulikana kama "Rock City" yani jiji la mawe. Mji wa Mwanza una mandhari nzuri sana ambapo Shule yetu (Mwanza Istiqaama Pre and Primary School) inapatikana.
Shule yetu (Mwanza Istiqaama Pre and Primary School) ipo katika wilaya ya Ilemela barabara ya Airport kilometa 10 kutoka mjini. Shule yetu ina mandhari nzuri na rafiki kwa mwanafunzi kujifunza, Shule yetu ina Walimu weledi waliobobea katika taaluma mbalimbali, pia tuna mazingira mazuri ya michezo ambayo wanafunzi wetu hufurahi wakiwa katika michezo mbali mbali.
Usafiri wa uhakika wakati wote amabao huwachukuwa Wanafunzi wetu kutoka majumbani kwao hadi Shuleni kwa salama na kwa wakati. Tuna dereva mahiri wenye utambuzi mkubwa katika udereva pia ni weledi katika kujumuika na Wanafunzi muda wote wanapokua safarini.
Tunapenda kuchukua nafasi hii adhimu kuwakaribisha katika Shule yetu, nafasi za masomo zipo wazi, jiunge leo uone tofauti kubwa, tunaamini hutokuja kujutia.
Hizi ni baadhi ya picha za Shule yetu karibuni sana.

Thursday, October 3, 2019
ZIARA YA KASA ZOO

Ilikua siku ya tarehe 30/05/2019 siku ya Ijumaa, ambapo walimu, wanafunzi na wafanyakazi wote wa shule ya Mwanza Istiqaama Pre & Primary School walijumuika katika safari ya kimasomo kuelekea "KASA ZOO" jijini Mwanza.
Ilikua safari nzuri na salama ambapo wanafunzi walifurahi pamoja na walimu wao na kujifunza vitu mbali mbali vinavyohusu wanyama pori na wanyama wanaofugwa nyumbani. Wanafunzi walipata kuona kwa mara yao ya kwanza wanyama wakubwa na wadogo wa porini na kustaajabu sana! Waliona farasi, ngamia, punda milia, kobe, sungura, nyoka wakubwa na wadogo, ndege aina nyingi na namna waoishi.
Pamoja na yote hayo, wanafunzi wetu walipata sehemu nadhifu na ya utulivu iliyo wawezesha kujumuika na walimu wao kula na kunywa na kupeana zawadi, pia wanafunzi walipa fursa ya kuuliza maswali mbali mbali yanayohusu wanyama, mfano mwanafunzi mmoja aliuliza
Ilikua safari nzuri sana, hizi ni baadhi ya picha zetu."Yule mamba kafa? Kiongozi wa ziara alimjibu kua mamba akishiba hulala hadi masaa 48!"